• Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada¬† kupitia Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo.
  • ¬†Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake nane; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi hivyo, watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi zetu wanachuo wa ufadhili binafsi watakaopenda kukaa nje ya Kampasi wanaruhusiwa.
  • Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha nne wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada (Cheti). Pia vijana waliomaliza Kidato cha sita na wale wenye Astashahada (Cheti) katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba wanakaribishwa kwa ajili ya kujiunga na mafunzo kwa ngazi ya Stashahada (Diploma)…

Tanganzo la Mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada  2018/19