Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kupitia Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo,Katika mwaka wa masomo wa 2018/2019 Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake nane; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi kwa sasa hivyo, watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi za wakala wanachuo watakaopenda kukaa nje ya Kampasi wanaruhusiwa.Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada na Stashahada. Pia wahitimu wa Astashahada wenye fani zinazohusiana na kozi wanazoomba wanakaribishwa kujiunga kwa ngazi ya Stashahada.

Application Form for Admission 2018/19