MKANDARASI ATAKIWA KUFUATA TARATIBU NA KANUNI UJENZI WA MAJENGO YA MIHADHARA.

Imewekwa: 30, September 2021

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA)Dkt. Pius Mwambeneametaka ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara katika chuo hicho Tawi la Tengeru Mkoani Arusha kujengwa kwa kufuata taratibu na kanuni za ujenzi.

Dkt. Mwambene amebainisha hayo leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo katika jengo la NBC jijini Dodoma, wakati wa utiaji saini wa ujenzi wa vyumba hivyo.

Ameaema anatarajia kazi ya ujenzi itatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Ameongeza kuwa mkataba unaonyesha muda wa ujenziuliopangwa ni miezi sita, ambapo ujenzi utaanza mwishoni mwa mwezi huu wa Septemba na kukamilikamwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka 2022.

Aidha Mtendaji huyo amesema kuwa gharama za ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara ni Shilingi Milioni 800 hadi utakapokamilika.

Awali akiongea baada ya zoezi la utiaji saini kukamilika Mkurgenzi wa Idara ya Utafiti, Ugani na Mafunzo Dkt. Angelo Mwilawa ameitaka kampuni ya LI JUN Devolopment Co Ltd ya Moshi inayotekeleza ujenzi huo, kufuata taratibu zote zilizoainishwa kwenye mkataba ili kupata matokeo bora yenye tija.

Naye meneja wa kampuni hiyo Bw. Xu Geng Sheng amewahakikishia viongozi na wataalam wa wizara waliokuwepo kwenye tukio hilo kuwa utekelezaji wa ujenzi huo utazingatia weledi na taratibu zote zilizopo ili kupata matokeo yenye tija na hatimaye kutangazavyema jina la kampuni.

Kwa wakati mwingine Mtendaji wa Mkuu wa LITADkt. Mwambene amesema vyumba hivi vinajengwa ili kupanua wigo wa udahili wa wanafunzi kukidhi uhitaji wa elimu kwa sasa hususan katika Sekta ya Mifugo.

Mwisho.