WANAFUNZI LITA WATAKIWA KUJIAJIRI

Imewekwa: 29, October 2021

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki ametoa wito kwa Wakala wa Vyuo vya mafunzo ya mifugo (LITA) kuongeza wigo wa utoaji Mafunzo kwa wafugali ili wawe na mtizamo wa kufuga kisasa na kupata faida zaidi.

Mhe. Ndaki amesema hayo alipotembelea LITA kampasi ya Tengeru,Wilayani Arumeru ambayo ni miongoni mwa kampasi nane nchin, ambapo ameihimiza LITA mbali na kutoa Mafunzo kwa Wanafunzi, iweke pia mazingira rafiki na rahisi ya utoaji elimu kwa wafugaji ili waelewe na kufanya ufugaji wa kisasa wenye tija kwa mfugaji na katika uchumi wa Taifa"ufugaji unaenda pamoja na malisho hivyo LITA tumieni mashamba darasa yenu kuwaelimisha wafugaji upandaji wa malisho ya mifugo yao "amehimiza Mhe.Ndaki

Vilevile Mhe.Ndaki ametoa wito kwa LITA kuwajenga wanafunzi wa Vyuo vya mifugo katika misingi ya kujiajiri pindi watakapo hitimu ili kuwa na wafugaji wenye ujuzi katika jamii ambao watahamasisha ufugaji wa kisasa na Wenye tija zaidi

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango amepongeza LITA Tengeru kwa kutumia mapato yake ya ndani kuboresha miundombinu , ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike iliogharimu Milioni 166.3 ambayo imezinduliwa na Mhe.Waziri Ndaki"kipekee niwapongeze Sana LITA Tengeru kuongeza mapato yake ya ndani kutoka Bilioni 3 hivi hadi kufikia zaidi ya Bilioni 4 "amesema Ruyango

Meneja wa LITA Tengeru Janeth Bendera amesema mbali na mafanikio makubwa ya kuwa na ongezeko la wanafunzi wanaojiumga na LITA Kampasi ya Tengeru kutoka 657 mwaka 2018/2019 hadi 1,579 Mwaka 2020/2021 Kuna upungufu wa miundombinu na mingi ni chakavu .

Aidha Mhe.Ndaki mbali na kuzindua hosteli ya wanafunzi 80 wa kike , ametembelea ujenzi wa vyumba vya Madarasa ,ukarabati mkubwa wa Maabara mbili za parasatioloji na multipurpose pamoja na eneo la upandaji malisho ya mifugo