Maombi ya Kujiunga na Chuo 2025-2026

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

WAKALA YA MAFUNZO YA MIFUGO

TANGAZO LA MAOMBI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA MIFUGO

Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kupitia Kampasi zake za Tengeru, Buhuri, Mpwapwa, Morogoro, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya mifugo, katika mwaka wa masomo 2025/2026

Kozi zitolewazo ni:

1. Astashahada na Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo

2. Astashahada na Stashahada ya Teknolojia ya Maabara ya Wanyama

3. Astashahada na Stashahada ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Teknolojia ya Vyakula vya Mifugo

Sifa za waombaji

  • Wawe wamehitimu Kidato cha Nne na kufaulu angalau masomo manne kwa alama D na kuendelea. Kati ya masomo hayo mawili yawe ya Sayansi ambayo ni Biolojia, Kilimo, Kemia, Fizikia, Hisabati na Jiografia

AU

  • Kidato cha sita wenye subsidiaries mbili za masomo ya sayansi

AU

  • Wahitimu wa kidato cha nne waliojiendeleza katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) vyenye mkondo wa mifugo na kupata NVA Level 3 au Trade Test I.

Kozi zote zinazotolewa na LITA zinakidhi vigezo vya kupata mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://olas.lita.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11 Julai, 2025.

Kwa mawasiliano zaidi tumia namba zifuatazo: 0742 762 364; 0767 775 146; 0714 994 755; au 0754 828 688

AU tembelea Tovuti ya Wakala: www.lita.go.tz

WOTE MNAKARIBISHWA