JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
WAKALA YA MAFUNZO YA MIFUGO
TANGAZO LA MAOMBI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA MIFUGO KATIKA KAMPASI ZA LITA, KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027
Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inawatangazia wahitimu wa kidato cha Nne na Sita wenye sifa kuomba kujiunga na kozi mbalimbali za mifugo zinazotolewa katika Kampasi za Tengeru, Buhuri, Mpwapwa, Morogoro, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula.
Kozi zinazotolewa ni kama ifuatavyo:
1. Astashahada na Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo
2. Astashahada na Stashahada ya Teknolojia ya Maabara ya Mifugo
3. Astashahada na Stashahada ya Usimamizi wa Nyanda za Malisho na Teknolojia ya Vyakula vya Mifugo
KOZI ZOTE ZINAZOTOLEWA NA LITA ZINAKIDHI VIGEZO VYA KUPATA MKOPO UNAOTOLEWA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU.
Sifa za Waombaji
Wawe na Elimu ya Kidato cha Nne na kufaulu angalau masomo manne kwa alama D na kuendelea, isipokuwa masomo ya Dini na Upishi. Kati ya masomo hayo mawili yawe ya Sayansi ambayo ni Biolojia, Kilimo, Kemia, Fizikia, Hisabati au Jiografia.
AU
Elimu ya Kidato cha Sita na angalau subsidiaries mbili za masomo ya sayansi,
AU
Elimu ya kidato cha nne na kujiendeleza katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) vyenye mkondo wa mifugo na kupata NVA Level 3 au Trade Test I
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yafanyike na kutumwa kwa njia ya mtandao kupitia: https://olas.lita.go.tz au fika katika kampasi ya LITA iliyo karibu nawe kwa msaada zaidi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10/07/2026
Wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya mifugo katika kampasi za LITA kupitia dirisha la OR-TAMISEMI watahitajika kuthibitisha na kupakua fomu ya maelekezo ya kujiunga na mafunzo kupitia Tovuti: www.lita.go.tz
Kwa mawasiliano zaidi tumia namba zifuatazo: 0666006070, 0794406611, 0714994755, Au tembelea tovuti ya LITA.
WOTE MNAKARIBISHWA