UZINDUZI WA HOSTELI LITA KAMPASI YA MOROGORO

Imewekwa: 16, April 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amezindua bweni la wanafunzi wa kike katika chuo cha Wakala ya Mafunzo ya Vyuo vya Mifugo(LITA) Kampasi ya Morogoro lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216 lililogharimu zaidi ya shillingi milioni 970 fedha za mapato ya ndani.

Akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo Aprili 06, 2024, Prof Shemdoe ameipongeza LITA kwa kufanikisha ujenzi huo kwa kutumia fedha za ndani ambapo kukamilika kwake kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondakana na changamoto ya mabweni kwa wanafunzi katika kampasi hiyo.