Mafunzo ya muda mfupi kwa wafugajji

Bonyeza hapa kupakua habari za mafunzo ya wafugaji

TANGAZO LA MAFUNZO YA MUDA MFUPI KWA WAFUGAJI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) imeandaa mafunzo ya muda mfupi kwa wafugaji kuhusu mbinu za ufugaji bora wa mifugo. Mafunzo hayo yatatolewa kwa siku saba (7) kwa kila kozi, kuanzia tarehe 21/09/2020 hadi 17/10/2020. Mafunzo yatatolewa katika kampasi za Tengeru, Kikulula, Morogoro, Mpwapwa, Madaba, Mabuki, Temeke na Buhuri.

Wafugaji watakaopata mafunzo katika awamu ya kwanza wanatakiwa kuripoti katika Kampasi hizo tarehe 20/09/2020.

Mafunzo yatakayotolewa katika awamu ya kwanza ni kama ifuatavyo:

Gharama kwa kila mshiriki kwa siku 7 ni shilingi 210,000/= kwa ajili ya malazi, chakula, mafunzo, shajala na ziara fupi za mafunzo.

Hata hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itamchangia kila mfugaji atakayehudhuria mafunzo katika awamu ya kwanza shilingi 70,000/=. Hivyo, mfugaji atachangia shilingi 140,000/= tu.

Kwa maelezo zaidi tumia namba zifuatazo: 0754 746 782; 0754 828 688, 0754 015 035 AU kwa njia ya Tovuti ya Wakala: www.lita.go.tz / www.mifugouvuvi.go.tz

WAFUGAJI WOTE MNAKARIBISHWA

Tanzania Census 2022