Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameitaka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) kuendelea kuboresha mafunzo na kutoa wataalamu wenye uwezo wa kukabiliana na mahitaji na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya mifugo nchini.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) pamoja na kikundi rika cha jamii ya wafugaji wa kata ya Samunge (Erumasidai) wamekuja na Mkakati mpya wa kujenga
​Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) imeendelea kuimarisha utoaji wa elimu kwa wafugaji nchini kupitia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu yanayotolewa katika kampasi zake pamoja na kuwafuata wafugaji moja kwa moja kwenye maeneo yao ili kuwajengea uwezo wa kufanya ufugaji wa kisasa na wa kibiashara.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, amewataka Watumishi wa Taasisi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uweledi, ubunifu, uchapakazi na uhadilifu mkubwa ili kuweza kuleta matokeo chanya katika Taasisi yao na Sekta ya Mifugo kiujumla.